JPIC
|
|
UMAHIRI WA UUMBAJI
SUALA
LA
WAUMINI WA LEO
ONGEZEKO LA JOTO
NA
MABADILIKO YA HALI YA HEWA ULIMWENGUNI
Prepared by the Global Warming Working Group of the JPIC Promoters,
Rome, Italy
If you want to send your comments, questions or would like more
information, please contact us at:
svd.jpic@verbodivino.it
http://www.svdcuria.org/public/jpic/index.htm
|
Athari katika maisha kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Utangulizi:- Jarida hili linalenga kutoa ufafanuzi kuhusu mabadiliko ya
hali ya hewa na ongezeko la joto katika ulimwengu. Pamoja na mbinu za
kukabiliana na hali hiyo mahali ulipo, kimkoa na kitaifa. Ni mategemeo
yetu kuwa jarida hili litakusaidia kuelewa vyema ukubwa wa tatizo hili,
pamoja na umuhimu wa kuchukua hatua za kuokoa ulimwengu wetu.
Tumetumia pia injili na teologia ambazo zitasaidia kuelimisha vikundi
na jamii kwa ujumla. Hatusemi kwamba jarida hili linaufafanuzi na majibu
yote kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na ongezeko la joto ulimwenguni,
bali linasaidia kuelewa ni wapi upate habari za awali zitakazo kuwezesha
kuchukua hatua zinazofaa ili kushughulikia jambo hili.
Jarida litajaribu kujibu maswali yafuatayo:
Ongezeko la joto na mabadiliko ya hali ya hewa duniani inamaanisha
nini?
- Ongezeko la joto hilo husababishwa na nini?
- Linaathiri vipi haki za jamii
- Athari zake ni zipi?
- Ni kwanini madhehebu ya dini yahusishwe katika mambo hayo?
- Imani yako inasemaje kuhusu viumbe na mazingira?
- Tufanye nini sasa?
Tafsiri ya mabadiliko ya hali ya hewa na ongezeko la joto duniani ni
ipi?
Kiasi cha kemikali katika anga hutegemea na viwango vya gesi iliyopo,
ambayo ni pamoja na kaboni dayoksaid, methane, na nitrous oxide. Hizo
ndizo zinazodhibiti joto.
Nishati ya jua ndiyo inayosukuma hewa na upepo duniani. Hiyo ndiyo
inayosababisha joto kwenye udongo na ardhi ambayo nayo hulirudisha joto
hilo kwenye anga. Gesi kutoka kwenye anga (mvuke wa maji, carbon dioxide,
n.k.) hudhibiti baadhi ya mishati na hubana kiasi Fulani cha joto. Kama
pasingekuwepo na udhibiti huo, kiwango cha joto kingekuwa cha chini kuliko
kilivyo sasa hivi, na maisha yasingekuwepo kama tunavyoyafahamu sasa hivi.
Tushukuru kuwepo kwa hali hiyo ya udhibiti wa joto kwa vile kwa wastani
kiwango kilichopo hapa duniani ni 60F/15C.
Hata hivyo, huenda pakatokea matatizo iwapo hali ya joto itaongezeka.
Tangu yalipoanza kutokea mabadiliko ya viwanda mlundiko/ongezeko la carbon
dioxide limepanda kwa asilimia thelathini (30%) na kiasi cha methane nacho
kimeongezeka mara dufu. Wakati huo huo, nayo nitrous oxide imeongezeka kwa
asilimia kumi na tano (15%). Hali hiyo imeongeza uwezo wa kudhibiti
ongezeko la joto katika anga ya dunia. Ongezeko hilo limesababishwa na
kitu gani? Wanasayansi huchukulia kuwa hayo hutokana na matumizi ya visiki
pamoja na shughuli nyingine za watu.
- Mabadiliko ya hali ya hewa ni mojawapo kati ya changamoto nzito sana
inayokabili dunia katika Karne hii ya ishirini na moja (21).
- Umepatikana ushahidi mzito kutokana na tafiti zilizofanyika hivi
karibuni zinazoonesha kwamba ongezeko la joto katika kipindi cha miaka
(50) hamsini iliyopita inatokana na shughuli za binadamu.
- Ongezeko la joto kwa kipindi kijacho litakuwa kubwa kuliko
ilivyofikiriwa/tarajiwa hapo awali.
Utafiti mwingi ambao umefanyika kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa,
unaonesha dhahiri kwamba hatutaweza kuepuka ongezeko la hali ya joto hapa
duniani, na inaelekea kuwa mabadiliko hayo ya hali ya hewa yamekwisha anza
kutokea. Mwezi Desemba 1977 na pia Desemba 2000 jopo la viongozi/watendaji
wa Serikali kuhusu mabadiliko ya Hali ya Hewa (IPCC) ambacho hushirikisha
wanasayansi wa kimataifa zaidi ya 2000, hufafanua kuhusu hali halisi
iliyopo sasa hivi.
- Kutakuwepo na ongezeko la maafa makali na mengi, ikiwepo pamoja na
matetemeko ya ardhi, mafuriko, vimbunga na ukame. Maafa makubwa kutokana
na hali mbaya ya hewa yameongezeka mara nne tangu mwaka 1960.
- Hali ya joto duniani inaweza ikaongezeka kwa wastani wa sentigeti 5 sawa
na farenhaiti 10 kufikia karne ijayo. Hata hivyo, joto hilo linaweza kuwa
kali zaidi katika baadhi ya nchi/ sehemu za dunia. Barafu ya Arkitik
imeyeyuka kwa kiasi kikubwa.
- Ukataji wa misitu ambao huzalisha hewa ya carbon na pia hupunguza uwezo
wa kunyonya carbon huchangia asilimia ishirini (20%) ya uzalishaji wa gesi
hiyo ya carbon ambako husababisha mabadiliko ya hali ya hewa.
- Tangu kipindi cha Vita ya Pili ya Dunia idadi ya magari duniani
yameongezeka kutoka milioni arobaini (40) hadi kufikia milioni mia sita
themanini (680). Moshi utokanao na magari huchagia gesi ya carbon dioxide
ambayo huzalishwa na watu na kuisambaza angani.
- Katika kipindi cha miaka hamsini (50) iliyopita tumemaliza asilimia
hamsini ya vyanzo vya nishati na tumeangamiza asilimia hamsini (50) ya
misitu ya dunia nzima.
Chanzo cha ongezeko la joto duniani ni nini?
Ongezeko la joto duniani husababishwa na ongezeko la aina Fulani ya
gesi ambayo imepewa jina la gesi ya nyumba ya kijani (Greenhouse) au GHG
kutokana na shughuli mbalimbali za watu na pia viwanda, hasa zile za CO2
na CFC. Gesi kubwa ya GHG ni carbon dioxide ambayo hutokana na matumizi ya
mkaa, petroli na gesi pamoja na kukata na kuangamiza misitu. Moshi
unaotolewa na magari pamoja na viwanda una gesi inayoitwa Nitrous Oxide,
ambapo gesi aina ya mehone hutokana na uzalishaji viwandani na kilimo. CFC
inauhabirifu mkubwa sana wa hewa na huchochea kwa kiwango kikubwa cha
ongezeko la joto duniani. Hata hivyo, gesi hizi sasa huondolewa kwa
kuzingatia makubaliano yaliyofanyika Mjini Montreal (Montreal Protocol) .
Carbon dioxide, clorofluoro carbons, methane, nitrous oxide ni aina ya
gesi ambayo hujaa angani na husababisha kuongezeka kwa joto linalotokana
na jua. Pamoja na kwamba bahari na mashamba huvutia kiasi kikubwa sana cha
CO2 uwezo wake wa kuhifadhi CO2 ni mdogo ukilinganishwa na ule wa
kusambaza aina hiyo ya gesi. Kwa maana hiyo, mlundiko wa GHG unaobaki
katika anga huongezeka kila mwaka na hivyo kuzidisha kupanda kwa joto
duniani.
Matumizi ya nishati katika kipindi cha karne moja iliyopita
yaliongezeka kwa kiasi kikubwa sana. Asilimia sabini (70%) ya nishati
hutumika katika nchi zilizoendelea, ambapo asilimia 78% ya nishati hiyo
hutokana na kisukuku. Hali hiyo hujenga uwiano usio mzuri kiasi kwamba
baadhi ya mikoa huendelea kuwa maskini na wakati huo huo mikoa mingine
huzidi kuneemeka. Hata hivyo, kiwango cha fedha zinazopatikana ili
kuzalisha nishati mbadala (mionzi ya jua, upepo, maji) ambayo ingechangia
sana kupunguza matumizi ya nishati itokanayo na Jossils katika nchi
zilizoendelea na zile zinazojikongoja ni kidogo mno ikilinganishwa na
misaada ya fedha inayotolewa katika uwekezaji wa miradi ya mafuta ya
fossils na nishati ya nuklea.
Ukatiji wa miti ya misitu ambayo ndiyo hunyonya carbon, husababisha
ongezeko la asilimia ishirini (20%) ya usambazaji wa hewa chafu aina ya
carbon, huharibu vyanzo vya maji na virutubisho vya ardhi (soil fertility)
Ili kuepusha mabadiliko mabaya ya hali ya hewa, pana umuhimu wa
kuimarisha kiwango kilichopo cha GHG katika anga mapema sana, na kwenda
sambamba na upungazaji wa asilimia hamsini (50%) wa gesi chafu za GHG kwa
kulingana na IPCC. Iwapo haya hayatatekelezwa, basi baadhi ya athari
zinazoweza kutokea ni hizi hapa.
Athari:
|
Ongezeko la kiwango cha maji ya bahari kutaathiri sana binadamu.
Watakaokumbwa zaidi na athari hizo ni wale ambao huishi kwenye visiwa
ambavyo havijainuka ya kutosha, wale waishio kwa wingi katika maeneo ya
pwani ya bahari na maziwa; kwenye mabonde ya mito n.k. Wengine ni wale
ambao huishi kwenye majangwa na maeneo ya mafuriko. Inakisiwa kuwa ifikapo
mwaka 2020 robo tatu ya watu waliopo duniani huenda wakaathirika na
mafuriko au ukame. Nchi zilizo maskini zitaathirika na mabadiliko ya hali
ya hewa kwa kiasi Fulani kutokana na hali yao kijiografia na pia
kutokuwepo kwa uwezo wa raslimali ambazo zingewawezesha kuizoea hali hiyo
ya mabadiliko kimaisha na pia kupunguza ugumu/makali ya maisha. |
|
Binadamu pamoja na viumbe wengine, tayari wanaathirika kutokana na
mabadiliko ya hali ya hewa. Utabiri wa wanasayansi unaelezea kuongezeka
kwa mateso na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, ikiwa ni pamoja na
kuumizwa na joto, ongezeko la maradhi yatokanayo na wadudu katika nchi za
tropiki kaskazini na kusini mwa ikweta na pia upungufu mkubwa wa
upatikanaji wa chakula (food insecurity). |
|
Hasara za kila mwaka kutokana na ongezeko la joto duniani linaweza
likafikia bilioni mia tatu za dola za kimarekani $300 bilion miaka hamsini
kuanzia sasa iwapo hatua thabiti hazitachukuliwa kudhibiti kuenea kwa hewa
chafu aina ya nyumba ya kijani (Greenhouse Gas). Iwapo viongozi wetu wa
kisiasa na watunzi wa sera hawatachukua hatu za haraka kukabiliana na hali
hiyo, basi uchumi wa dunia huenda ukaathirika sana. Katika kipindi cha
miaka kumi iliyopita, majanga yaliyotokea yameleta hasara kwa dunia
inayofikia dola za kimarekani bilioni mia sita na name ($608 billion) |
|
Mradi wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (UNEP) kupitia mwakilishi wake
kwenye mkutano wa saba juu ya mabadiliko ya Hali ya Hewa (COP7)
uliofanyika Novemba 2001 Marakech nchini Morrocco ulielezea kwamba baadhi
ya mazao muhimu ya kilimo, ikiwemo ngano, mpunga, na mahindi, huenda
uzalishaji wake ukapungua kwa asilimia 30% kwa kipindi cha miaka mia moja
ijayo kutokana na ongezeko la joto duniani. Wanahofia kwamba wakulima
ambao watakuwa wamekata tamaa, watahamia sehemu za milimani ambako kuna
baridi na kuvamia misitu nyeti na hivyo kuhatarisha maisha ya wanyama pori
na vyanzo vya maji pamoja na ubora na uwingi wa maji hayo. Utafiti huo
unaonyesha kwamba tayari idadi kubwa ya watu wanaoishi katika nchi
zinazoendelea wana upungufu mkubwa wa chakula, lishe duni na utapia mlo. |
Wakibimbizi kutokana na uharibifu wa mazingira dunia nzima sasa hivi ni
milioni 25 |
Maswali ya kutafakari:
- Kuna lolote jipya katika haya yaliyoelezwa?
- Hali hii imekugusa vipi wewe binafsi?
Hali ya wasiwasi iliyopo sasa hivi katika sayari hutokana na ulaji
mwingi siyo kwa asilimia themanini ya maskini waliomo katika sehemu mbili
kati ya tatu za dunia Bali ni kwa wale matajiri ambao ni asilimia ishirini
na hukwapua asilimia themanini na sita ya raslimali za dunia. |
Dini/Imani yetu ya kimila inasemaje?
Ili iweze kuaminika, teologia kakamavu hapana budu iwe na misingi ya
elimu ya sayansi kuhusu ukubwa na uzito wa safari za ulimwengu.
Mtakatifu Bonaventura kwa kuzingatia uzoefu wa Mtakatifu Francis
alifafanua teologia ya sakramenti ya kuumba ambazo ndizo ni nyayo za Yesu
Kristo katika dunia iliyoumbwa. Dunia inakaliwa na Watakatifu. Viumbe wote
ni alama na ufumbuo kuhusu Muumbaji anayeacha/weka alama kila mahali.
Kuharibu kwa makusudi kipengele chochote cha uumbaji, ni sawa kabisa na
kufuta sura ya Kristo ambayo ipo katika viumbe wote. Kristo huteseka siyo
tu pale watu wanaponyimwa haki zao na kudhulumiwa, bali pia wakati bahari,
mito na misitu inapoharibiwa. Pale uumbaji unachukuliwa kuwa ni
sakramenti, ikituonesha na kutuongoza kwa Mungu; basi uhusiano wetu na
watu wengine unapewa changamoto tuhame kwenye ukandamizaji na ubabe na
kwenda kutoa heshima za hali ya juu.
Kwa nini dini zizingatie na kujihusisha na mambo ya mazingira na
viumbe?
Dunia inauwezo mkubwa wa kukabiliana na maumivu, lakini kamwe haiwezi
kuendelea kufanya hivyo bila mwisho bila kuhatarisha uhai wa ubinadamu.
Tupo katika nafasi ya kuweza kufanya jambo Fulani.
Hati maalum ya Baba Mtakatifu ambayo inaelezea kiundani juu ya maswala
ya mazingira na maendeleo yenye kichwa kisemacho “Amani na Mungu Muumbaji,
Amani na viumbe wote” ya 01 Januari 1990 inatoa changamoto kuwa “Wakristo
kutambua kuwa wajibu wao kwa mazingira na viumbe ni kipaumbele cha imani
yao”.
Umilikaji wa dunia kwa Mungu unatuhimiza siyo tu haki za kijamii, yaani
uhusiano kati ya watu, bali pia haki ya kimazingira na viumbe vingine na
ardhi yenyewe. Uumbaji unaeleweka kuwa ni jamii ya viumbe walioshikamana
na kuungana na Mungu na Mazingira thabiti ni sehemu muhimu ya imani zote
na ni jambo la muhimu kulizungumza, kushirikiana na kuelewana.
Makanisa na vikundi mbalimbali vya kidini tayari vinahusika sana na
hali ya mazingira na viumbe, na ni muhimu kuwasiliana na wakristo wengine
pamoja na wasio Wakristo, kuhusu jambo hilo la mazingira na viumbe.
Hii ndiyo changamoto ya leo:
|
Sisi ni watu tunaoweza kuziona na kusoma “alama za wakati” |
|
Tumejifunza kuhusu mambo ya kuchambua/ kuchunguza. |
|
Tunazo raslimali na tumeunda mtandao wa mawasiliano na tahadhari juu ya
ongezeko la joto duniani. |
|
Kwa kuzingatia wito wetu wa kiroho na ukarimu, tunajizatiti kusuluhisha
na kurejesha amani na maelewano. |
|
Tunaitwa kuchagua wadhifa wa unabii |
|
Sisi ni wanadamu wenye asili ya maadili ya wema na kuwaunga na kutoa
msaada kwa watu wanaoumwa na wanaohitaji kutunzwa. |
Wajibu wetu, kama wanaume na wanawake wa dini, ni kutafakari uzuri na
uwepo wa Mwenyezi Mungu katika mambo yote. Tafakari hizo hutuwezesha
kurekebisha mioyo yetu ili tuweze kukabiliana na matatizo yoyote kwenye
sayari na nyumba zetu. Uumbaji wa Mwenyezi Mungu ndiyo sura za mwanzo wa
milenia mpya.
Majibu yetu yatazingatia/yatategemea na mazingira ya mahali tunapoishi.
Kwa wale ambao huishi kwenye nchi na jamii zinazopenda ulaji mkubwa na
kuthamini mali, mbinu zao za kuishi kwa amani na upendo zitakuwa tofauti
na zile za watu wanaoshi katika jamii na nchi ambazo hazina vitu ambavyo
ni muhimu katika kumwezesha mtu kuishi kwa heshima.
Maswali ya kutafakari:
- Kwa nini dini zijihusishe katika mambo ya mazingira?
- Kuna sababu yoyote ambayo inailazimisha dini (madhehebu)
kujihusisha na mambo ya mazingira?
- Kaka na dada zako huwa na msimamo gani unapozungumza nao kuhusu mambo ya
mazingira?
Msimamo Wa Kikristo Kuhusu Maadili Ya Mazingira
Mambo muhimu katika maadili ya Umoja hujumuisha haya:
- Kutambua na kukubali thamani ya uumbaji,
- Kutambua kuwa mazingira ni kati ya vitu vyenye manufaa kwa jamii/umma
- Miundo ambayo ina manufaa kwa umma
- Uwiano kati ya mazingira na maendeleo.
Maadili mema kuhusu mazingira yetu maisha pia ukuzaji wa uchumi pamoja
na viumbe.
Jambo la msingi katika maadili ni kutambua na kuyajali yale mengine
na vipi niwajibike kwa hayo mengine. |
Kumtabua na kumthamini mtu, hapana budi mimi mwenyewe nirekebishe tabia
yangu ili niweze kumheshimu na kumjali hata mtu mwingine. Tendo/tabia ya
kushusha hadhi ya viumbe wengine kunachangia kwa kiasi kikubwa sana
kuharibika kwa mazingira. Maoni ya kimaandishi ya Mtakatifu Francis,
Hildegard wa Bingen pamoja na methali nyingine nyingi huonesha kwamba
kuumba kuna uzito, wake wa kipekee wa kimaadili ambao Mwenyezi Mungu
amependa uwepo.
Tunafahamu kwamba kuna mema yanayopendwa kimataifa ambayo huvuka
mipaka ya Kitaifa. |
Hali njema ya bahari, misitu, anga, wanyama, samaki na aina mbalimbali
ya mimea ni suala ambalo linatiliwa maanani sana hata nje ya mipaka ya
nchi na serikali zake. Maswali ya mazingira hutulazimu kufafanua kile
ambacho ni cha kwa manufaa kwetu kwa kuzingatia ulimwengu kwa ujumla.
Tunapotumia raslimali zetu kwa kasi na kwa kiwango ambacho hatuwezi
kurejesha tena raslimali nyingine bila kutilia maanani mahitaji ya vizazi
vijavyo, basi hapo huwa tunawaibia mitaji yao. Leonardo Boff anasema kuwa
utu ndio ufahamu wa dunia. Fikra hizo hutusaidia kutathmini upya uhusiano
baina ya viumbe wote. Ingawa binadamu ana nafasi na wajibu maalum katika
mipango ya Mungu hapa ulimwenguni, lakini binadamu hawezi kuishi kwa muda
mrefu hapa duniani kama hana uhusiano bora na mazingira yanayomzunguka.
Binadamu anahitaji viumbe ili aweze kuishi, ambapo viumbe hao wengine
hawamhitaji banadamu ili nao waweze kuishi.
Pana umuhimu wa kuweka mikakati ya kulinda na kuhifadhi mazingira ya
ulimwengu. Hii ina maana sharti tutilie maanani wito wa Baba Mtakatifu,
John Paul II alioutoa tarehe 17 Januari 2001 kwamba tuelewe kwa undani
zaidi mabadiliko ya hewa na mazingira.
Pana umuhimu wa kuwaelimisha watu kuhusu hali ya mazingira
inavyohatarisha sayari na pia siri kuhusu kuwepo kwa sayari yenyewe.
Madhehebu ya Dini yanaweza kutoa mchango gani kwa jambo hili?
|
Madhehebu ya dini yanaweza kubuni mbinu za kuhifadhi/ kutunza
rasilimali. Kujizatiti kwetu kuishi kijamii kunatupa nafasi ya pekee ya
kuhifadhi na kurejeleza (recycle). |
|
Baadhi yetu, ambao tunauelewa zaidi wa hali ilivyo, inawezekana tayari
tumebadilisha mtindo wetu wa kuishi (life style) na tumejihusisha kisiasa
na kwa lengo la kuleta mabadiliko. |
|
Kwa watu wengine, ujumbe na habari ambazo zimo kwenye jarida hili, ni
chanzo cha kuelewa umuhimu wa kukabili janga hili mapema iwezekanavyo. |
|
Madhehebu ya dini mara nyingi huwasiliana na mashirika yasiyo ya
kiserikali (NGOs) yanayojihusisha na mambo ya mazingira, na pia pana uwezo
wa kushirikiana nayo katika miradi yao au uhamasishaji wa jamii. Angalia
mtandao wa NGOs za nchi yako juu ya mabadiliko ya hali ya hewa. |
|
Waalike wanamazingira kwenye mihadhara mbalimbali ya kuwaelemisha
wananchi. |
|
Shirikiana kikazi na watu ambao hawana ardhi, waliotimuliwa, wakimbizi,
wenyeji na waunge mkono katika masuala ya ardhi, maji pamoja na misitu. |
|
Nini zaidi? |
Je, unafahamu kwamba ni mara ya kwanza sasa kuwepo kwa mkataba wa
kimataifa kuhusu hifadhi ya mazingira kwa lengo la kupunguza gesi ya
“Greehouse”. Mkataba huo hujulikana kama “Kyoto Protocol” na una nguvu za
kisheria. Hata hivyo, ili uweze kutumika, hapana budi uridhiwe na mataifa
55 ingawa hadi sasa ni mataifa 46 tu ambayo yameridhia. Hali kadhalika,
mataifa yakayoridhia mkataba huo, sherti miongoni mwao yawe asilimia 55%
ambayo hutengeneza gesi ya GHG. Yaani nchi zenye viwanda vingi. Hadi sasa
ni mataifa machache tu ambayo yameridhia mkataba huo. |
Binafsi na kujumuiya tunaweza kutekeleza hizo “R” ambazo idadi yake ni
tatu!
Rejeleza/ Tumia upya …..
|
Tuthmini na rejea upya matumizi/ununuzi wa vitu au usitumie vitu ambavyo
havijasindikwa au kuwekwa kiutaalaam katika vifurushi. Tafuta sabuni nzuri
ya kuoshea vyombo vya jikoni, kufulia nguo na vyombo vya usafishaji. |
|
Rejeleza kitu chochote ambacho kinaweza kufanywa hivyo; mfano ni
plastiki, matunda, mboga, karatasi, kadi, glasi na bakuli. |
|
Anzisha lundo la mbolea vundo na ongeza majani na takataka nyingine za
shambani ambazo zitaliwezesha lundo hilo la taka kuzalisha mbolea nzuri
sana za asilia katika ardhi yako. |
|
Wahamasishe wenye viwanja kuchukua majukumu ya kurejeleza au kutupa
vipuri ambavyo vimekwisha chakaa, mfano ni vile vya kompyuta na luninga
(TV) |
|
Nini zaidi? |
Punguza ……
|
Punguza matumizi ya maji |
|
Punguza matumizi ya gari lako |
|
Punguza uchomaji wa vitu ambavyo havijarejelezwa (recycled) |
|
Punguza uzalishaji wa moshi utokanao na CFC au mbadala wa CFC kwa
kutotumia aerosols ana tumia vifaa vinayotumia vyema mishati. |
|
Bana matumizi ya umeme kwa kutumia taa zenye tubu ndefu badala ya balbu
za kawaida. |
|
Nini zaidi? |
Kumbusha ……….
|
Zikumbushe Serikali za mitaa kuhusu kujizatiti katika kurejelesha na
kupunguza uzalishaji wa takataka pamoja na kuzingatia upya sheria zao juu
ya urejeleshaji na uondoaji takataka ili ziende na wakati. |
|
Wasisitize wasindikaji wa bidhaa kuhusu uwahisishaji wa kufunga vifushi
vya bidhaa zao. |
|
Wakumbushe viongozi juu ya kubana matumizi ya umeme na pia wawe na mfumo
bora wa umeme. |
|
Ikumbushe Serikali kuhusu kuwajibika kwake katika kutekeleza maazimio na
itikadi za kimataifa kuhusu mazingira. |
|
Wakumbushe unaokutana nao kila siku kuishi vyema ulimwenguni na pia
kuchambua/kupitia upya mtindo wao wa matumizi wa kile walicho nacho. |
|
Nini Zaidi? |
Wasiliana na Idara ya mazingira na wanasiasa wa nchini kwako. Waulize
wanafanya nini katika kutekeleza makubaliano ya Kyoto. Iwapo unaishi USA
ambayo imejiengua kutoka makubaliano hayo ya Kyoto, basi tuma barua kwa
Rais wa nchi hiyo ya USA na kumsihi afikirie kurudi upya kwenye
makubaliano hayo ya Kyoto. Wasiliana na Mratibu wa Umoja wa Mataifa ambaye
huwa kwenye ofisi ya UNDP hapo nchini kwako ili ujue umoja huo unaendesha
miradi gani hapa nchini inayohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa
ulimwenguni. |
Kutafakari Na Kusali
Ukisha maliza kulisoma jarida hili tunakushauri ujumuike na wenzio au
na marafiki ili mtafakari na kusali kwa pamoja.
Chagua ukumbi wa kawaida tu kwa ajili ya kusali huko – beseni la maji,
mshumaa na udongo.
Wito Wa Kusali
Hatimaye utunzaji wa mazingira ni wito wa kuwajali viumbe wote, na
kuhakikisha kuwa shughuli za watu ambazo hubadili ardhi haziathiri uwiano
bora uliopo kati ya viumbe wote ambao hutegemea ardhi, hewa, na maji kwa
ajili ya kijamii, kiuchumi na kisiasa kutokana na kuendelea kudorora kwa
mazingira ambako kunawaathiri sana maskini. Uwezekano wa mabadiliko ya
hali ya hewa na kuongezeka kwa maafa huzua maswali mengi kuhusu mwelekeo
wa jamii ya sasa hapa ulimwenguni. Ongezeko la ufa kati ya walio maskini
na matajiri usisababishe kutokujaliana na wala matumizi holela ya
raslimmali za dunia na kuongezeka na kupungua kwa viumbe wengine. Hii ni
kauli ya Kadinali Francois Xavier Nguyen Vau Thuau, Press Pontifical
Council for Justice and Peace.
Salini pamoja Zaburi 148 kipengele 1-10.
Tulia kimya na utafakali haya yafuatayo:
- Uliposoma jarida hili, ni nini hasa kilishokuvutia/hamasisha?
- Unao msimamo gani ndani yako?
- Umewahi kuziona dalili zozote hapo unapoishi za kuongezeka kwa joto la
dunia?
- Hati zenu (Katiba, Sharia n.k.) huzingatia vipi kujali viumbe?
- Mkutano wetu wa kitaifa wa Maaskofu umewahi kutoa kauli yoyote kuhusu
ongezeko la joto duniani?
- Linaagiza mambo gani Kanisa lenu hapo ulipo?
Wito wa vitendo:
- Utachukua hatua gani thabiti kuhusu ongezeko la joto duniani?
Sala ya mwisho
“Sifa zote zielekezwe kwako, Bwana Wangu, kupitia viumbe vyote
Na wa kwanza ni wewe Kaka yangu Jua, ambaye huleta siku ….
Ni mrembo sana na anameremeta!
Anafanana sana nawe.
Sifa zote zikuendee wewe Bwana kupitia dada yangu Mwezi na Nyota;
Umeviumba mbinguni, vinaag’ara vyenye thamani na safi.
Sifa zote zielekezwe kwako, ee Bwana, kupitia Kaka zangu, Upepo na Hewa….
Sifa zote zije kwako, ee Bwana, kupitia dada yangu Maji,
Ambaye hana mbwembwe, anafaa sana na hapendelei.
Sifa zote zije kwako ee Bwana, kupitia Kaka Moto,
Ambaye unamtumia usiku kuleta mwanga…
Sifa zote zielekee kwako, ee Bwana kupitia kwa Dada yetu Ardhi ambaye pia
ni mama yetu,
Ambaye hutulisha na huzalisha aina mbali mbali za matunda
Pamoja na maua na mimea….
Msifuni na mbariki Bwana na mpe shukrani
Na mtumikie kwa unyenyekevu mwingi.”
Kifupisho cha Wimbo Wa Solomon Kuhusu Viumbe (Mt. Francis Wa Asisi)
Ili uweze kupata habari zaidi na ulielewe ipasavyo jambo lenyewe na
hatua ambazo unaweza kuzichukua:
Chaguo la Tuvuti (website) na raslimali nyingine (nyingi ni za lugha
mbalimbali)
- Greenpeace: http://www.greenpeace.org/
- Climate Voice: http://www.climatevoice.org/
- “Earth Charter”- http://www.earthcharter.org/
- Friends of the Earth: http://www.foei.org/
- Planet Ark: http://www.planetark.org/index.cfm
- International Institute for Sustainable Development:
http://www.iisd.ca/
- Union of Concerned Scientists:
http://www.ucsusa.org/warming/index.html
- UN Framework Convention on Climate Change:
http://www.unfccc.int
- World Wildlife Fund: (simple explanation on climate change in four
languages)
http://www.panda.org/resources/publications/climate/crisis/crisis.htm
- UN Environment Program: http://www.unep.org
- UN Development Program:: http://www.undp.org
- Food and Agriculture Organisation; http://www.fao.org
- Alliance for Religions and Conservation:
http://www.religionandconservation.org
- Climate Action Network http://www.climatenetwork.org
- World Council of Churches Climate Change Programme: Dr. David G.
Hallman, WCC Climate Change Programme Coordinator, c/o The United Church
of Canada, 3250 Bloor Street West, Toronto, ON, Canada M8X 2Y4 Tel:
+1-416-231-5931 Fax: +1-416-231-3103 E-mail:
dhallman@sympatico.ca
Lugha mbalimbali
Kijerumani:
Kifaransa:
Kihispania:
Maandishi Matakatifu Ya Nyaraka Za Kanisa
- Mwanzo 1:1-2:3; 9:9-11
- Kutoka 3:7-10; 15:22-27; 23:10-12
- Mambo ya Walawi 25:1-24
- Hekima 11, 24-26
- Isaya 11:1-9; 40:12-31
- Danieli 3:57ff
- Zaburi 8; 19; 24; 104:16-23; 136; 148:1-4 & 7-10
- Mithali 8:22-31
- Marko 5:35-41
- Marko 12, 29-31
- Mathayo 5,1-14
- Mathayo 12,22-34
- Mathayo 6:26-30
- Luka 16:19-31
- Yohane 9; 12:23-26
- Waroma 8:18-25
- Wakolosai 1:15-20
- Ufunuo 21:1-5; 6:16-21
- Waroma 8, 22-24
- 1Kor. .3, 9
Nyaraka Za Kanisa Kuhusu Ekolojia
(Tafuta nyaraka za mikutano ya Maaskofu wa nchi yako pamoja na zile za
kutoka mikoani)
- Ujumbe wa Yohani Paul II (1 Januari 1990) kwa siku ya Amani Duniani: Amani
na Mwenyezi Mungu Muumbaji, amani na Viumbe wote.
- Catechism of the Catholic Church: 299-301; 307; 339-341; 344 2415-2418
- Encyclical Letter Populorum Progressio, 23, 24
- Encyclical Letter, Fides et Radio, 104
- Encyclical Centesimus annus, 37-38
- Encyclical Laborem exercens, 4
- Encyclical Mater et Magistra, No 196, 199
- Apostolic Letter Octogesima adveniens, 21
- Encyclical Redemptor hominis, 8, 15
- Encyclical Sollicitudo rei socialis, 26, 29, 34
- Apostolic Letter, Octogesima Adveniens, 21
Siku za kukumbuka Ekolojia na Mazingira
Mwezi Machi
22 |
Siku ya
Kimataifa kuhusu Maji |
Mwezi
Aprili 22 |
Siku ya
Dunia |
Mwezi Mei
22 |
Siku ya
Kimataifa ya Bilogia Mbalimbali |
Mwezi Juni
5 |
Siku ya
Ulimwengu kuhusu Mazingira |
Mwezi Juni
17 |
Siku ya
Kimataifa ya Kupambana na Uletaji Jangwa |
Mwezi
Septemba 16 |
Siku ya
Kuhifadhi Tabaka la Hewa ya Ozone. |
Iwapo ungepeda kuchangia mawazo au kukosoa
kijarida hiki, wasiliana na Mratibu wako wa usharika kuhusu Haki na
Amani:
Michael Heinz
svd.jpic@verbodivino.it |
|